šWaajiriwa wapya 555 wapata ajira kwa mara moja
šMwenyekiti wa Bodi ya TANESCO afungua rasmi mafunzo elekezi kwa waajiriwa hao
Na: Mwandishi Wetu, Dodoma
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeandika historia kwa kuajiri watumishi wapya 555 kwa mara moja, hayo yameelezwa katika uzinduzi wa mafunzo elekezi kwa waajiriwa hao, huku Mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Rhimo Nyansaho, jijini Dodoma.
Mafunzo hayo yamefunguliwa tarehe 21 Julai, 2025 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, yakilenga kuwapa uelewa mpana kuhusu majukumu yao ndani ya Utumishi wa Umma na ndani ya Shirika, kabla ya kuanza kazi rasmi katika maeneo waliyopangiwa kote nchini.

Akifungua mafunzo hayo, Dkt. Nyansaho aliwataka watumishi hao wapya kutambua uzito wa fursa waliyoipata na kuitumikia kwa bidii, uadilifu, na uaminifu mkubwa.
āKipekee namshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kibali cha kuajiri. Hii ni fursa ya kipekee, na ni wajibu wenu kuithamini kwa kufanya kazi kwa juhudi na weledi mkubwa,ā alisisitiza Dkt. Nyansaho.
Akiwaasa kuhusu mwenendo wao wa kikazi, aliwakumbusha kuwa TANESCO imepiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma bora kwa wateja, hivyo wanapaswa kuendeleza juhudi hizo kwa kuwahudumia wateja kwa kuwajibika na kuwa na maadili ya hali ya juu.
āTumepiga hatua kwenye utoaji wa huduma bora kwa wateja, hivyo ni muhimu muiendeleze kwa kuwahudumia wateja kwa uaminifu na uadilifu kwa maslahi mapana ya Shirika na Taifa kwa ujumla” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, aliwataka waajiriwa hao kuwa mabalozi wa Shirika katika maeneo yao ya kazi kwa kutekeleza majukumu yao kwa bidii, uaminifu, na kwa kutoa huduma bora kwa wateja.
āKatika majukumu yenu, mnakwenda kukutana na wateja wetu. Wahudumieni kwa heshima na kwa moyo wa kujitolea, ili kwa pamoja tuendelee kujenga taswira chanya ya TANESCO,ā alieleza Bw. Twange.
Waajiriwa hao wameajiriwa na TANESCO hivi karibuni baada ya kupitia mchakato wa ajira, huku awali wakiwa wafanyakazi wa mikataba ya muda na ajira hizi mpya zinawapa fursa ya kupata ajira za kudumu.


