-Mtanange wa ufunguzi kupigwa uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia Aug 2, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Ikiwa ni maandalizi kuelekea michuano ya “African Nations Championship” CHAN Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 21,2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg Gerson Msigwa ofisini kwake Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao mambo kadha wa kadha yalijadiliwa kwa lengo la kujipanga kuweka mazingira rafiki ya michuano hiyo hapa nchini hususani Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa ni fursa adhimu ambayo Taifa imepata hivyo ni vema ikatumiwa vizuri kwa masilahi mapana ya ustawi wa jamii ya kitanzania kiuchumi.

Akiwasilisha taarifa ya maandalizi Ndg Gerson Msigwa amesema hadi sasa maandalizi yako vizuri katika nyanja mbalimbali ikiwemo maandalizi ya viwanja vya mazoezi kwa kuzingatia mahitaji ya mashindano hayo.

Naye Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila ameihakikishia kamati hiyo kuwa Mkoa uko tayari kushirikiana kamati maandalizi kufanikisha kwa viwango vya juu mashindano hayo ya CHAN.