Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Thabit Kombo amesema serikali imepata mkataba wa ajira 50,000 kama mchango wa Tanzania kwa nchi za nchi za nje.
Waziri Kombo ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan kwenye uwanja wa Buza-Tanesco wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam leo Oktoba 23,2025.
Leo tumemaliza vikao vyetu vya awali na wale wakaguzi wa kimataifa waliofika kuja kutuangalia demokrasia yetu na jinsi Tanzania inavyofanya eneo hili. Kuanzia kesho utaonana na viongozi hao ni wengi wamekuja kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni.
Jambo la pili, naomba nikujulishe kuna ahadi ulizitoa katika Ilani iliyopita na umezitimiza kwa asilimia kubwa na hadi katika Ilani ilani ijayo, wengi wanasema tutafanya, wewe umekwishafanya umetekeleza na unaendelea kutekeleza.
Hii ni taarifa njema ambayo nimeipokea leo ni suala la ajira kwa vijana wenye umri wa miaka 20 hadi 35. Katika Ilani iliyopita uliahidi nafasi za ajira milioni 5, katika ilani nyingine umeongezewa mpaka milioni 8, naomba kukwambia tumepokea mkataba leo chini ya serikali yako ajira ni zako 50,000, naomba mwenezi uje upokee mkataba huu uwasilishe kwa mwenyekiti wangu,amesema.
Amesema pia kuna ajira 20,000 na kuwataka vijana wa Tanzania kujitayarisha ndani ya nchi na nje ya nchi ambazo lazima utaratibu wake usimamiwe na serikali.
Mjitayarishe kwa wale ambao watafanya interview serikali yenu pamoja na chama chenu kitawasaidia mfaulu ili tusikose nafasi moja katika ajira hizi.
Ajira zingine 20000 ziko njiani kuja mwenyekiti, huu ndiyo mchango wetu kwa upande wetu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Sisi tunafanya kwa vitendo zaidi, hatusemi kwa meneno, Dk Samia anafanya kwa vitendo hafanyi kwa meneno na ushahidi ndiyo huu hapa ametimiza yak wake, kazi kwenu vijana,amesema.
