Na Jovina Massano

UJUMBE wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mhandisi Hamad Masauni ,umetembelea Bandari ya Oslo nchini Norway kwa lengo la kujifunza namna bandari hiyo inavyohifadhi mazingira na kuzuia uzalishaji wa gesi joto.

Akiupokea ujumbe huo vandarini hapo Mkurugenzi mkuu wa Bandari ya Oslo Bw.Ingvar M.Mathisen amesema Bandari chanzo kingine Cha biashara ya Kaboni.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Mhandisi Hamad Masauni akiwa na Mkurugenzi mkuu wa Bandari ya Oslo nchini Norway Bw Bw.Ingvar M.Mathisen.

Mkurugenzi mkuu wa Bandari Bw.Mathisen ameeleza kuwa Bandari ya Oslo ni bandari mtambuka na ya tatu kwa ukubwa duniani kwa kuwa ina teknolojia janja ya Bahari kwa kuwa haizalishi gesi joto.

Lengo kuu la bandari hiyo ni kuhakikisha kuwa inapunguza gesi joto kwa 80% ifikapo mwaka 2030 na serikali imeazimia kufikia lengo hilo kwa kutumia teknolojia.

Mwaka 2018 Bandari ya Oslo imeacha kupokea na kuendesha meli zake kwa kutumia mafuta na badala yake meli za abiria,mizigo na za starehe zote zinatumia umeme.

Kwa vyombo vyote ambavyo havitumii teknolojia ya umeme katika bandari hiyo hutizwa ada ya uzalishaji gesi joto(-Emission Fees)inayojumuishwa kwenye mpango wa biashara ya Kaboni.

Kupitia ziara hiyo Tanzania imebainisha fursa mbalimbali za uhifadhi na usimamizi wa mazingira kupitia uchumi wa bluu na biashara ya Kaboni.

Tanzania ni nchi ambayo Mashariki yake ina Pwani ndefu ya Bahari ya Hindi ambayo ina Bandari kubwa ya Dar es salaam, Mtwara na Tanga lakini pia kuna bandari ndogo zinazohifumia Lindi,Kilwa Masoko,Mafia,Pangani na Kwale.

Bandari zote hizi hutumia vyombo vya usafirishaji,hivyo kwa kuwa na teknolojia ya kutambua kila chombo huzalisha kiasi gani Cha gesi joto Mamlaka husika kwa kushirikiana na kituo Cha ufuatiliaji wa Kaboni NCMC zinaweza kufanya biashara hiyo kwa kudai ada ya uzalishaji gesi joto.