Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia
Dar es Salaam
WAKALA wa Majengo TBA imewataka Wapangaji wote wa nyumba za kuishi,Biashara,pamoja na wale wanaoishi kwenye Maeneo yao ambao wana madeni ya Kodi na malimbikizo ya nyuma kulipa kabla ya Septemba 30,2025 kwani baada ya muda huo kutisha zoezi la kuwandoa litaanza Nchi nzima .
Akizungumza leo Septemba 12,2025 Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Daud Kondoro amesema wadaiwa ambao hawatalipa madeni hayo ndani ya muda huo uliotolewa wataondolewa kwenye nyumba hizo au Maeneo hayo pamoja na kuchukuliwa hatua Kali za kisheria
“Hakuta kuwa na muda wa ziada baada ya Septemba 30,2025 wa kulipa madeni hayo hivyo nawasihi wadaiwa wote kuhakikisha mnalipwa madeni yote katika muda uliotolewa”amesisitiza Kondoro.

Mkurugenzi Kondoro amebainisha kuwa utaratibu wa kisheria kuwapangisha Watumishi wa Umma na watu binafsi wenye sifa nyumba za Serikali pindi zinapopatikana
Hivyo TBA inawataka Wapangaji wote waliopangishwa wakiwa na sifa na sasa wamekosa sifa za kuendelea kuishi kwenye nyumba hizo kukabidhi mara moja ndani ya kipindi kilichotolewa pamoja na kulipa malimbikizo ya Kodi ya pango
“Watumishi wa Umma waliohamia Vituo vipya vya kazi vilivyo nje ya Mkoa ambao wamepangishwa nyumba,Watumishi wa Umma waliostaafu kwa mujibu wa Sheria au hiari ,Ndugu wa Watumishi wa Umma Waliofariki ,Walioondoka kwenye utumishi”Amesema Mkurugenzi
Hata hivyo amebainisha kuwa kuna madeni yanayotokana na nyumba ambazo wamezipangisha kwa watumishi wa umma ambapo wapo watumishi 67 lakini tuna wapangaji ambao wamepangishwa kibiashaara na ni Wizara na taasisi za umma 12.

Naye Fredrick Mdeme Mkurugenzi wa idara ya miliki amesema mpaka sasa jumla ya fedha na deni la kodi ya pango ambalo linadaiwa ni kiasi cha shilingi bilioni nne milioni mia tano laki saba themanini na na senti kama themanini na tisa hizo ndizo fedha ambazo wanadai kwa wapangaji ambao wamepangishwa nyumba mbalimbali za Wakala wa Majengo Tanzania TBA.
“Kimsingi madeni haya yanahusisha tunafahamu ili mpangaji awe mdaiwa sugu deni lake linapaswa kuwa limekaa kwa kipindi cha miezi mitatu hivyo kama mpangaji hajalipa mwezi wa kwanza atapelekewa notisi atakumbushwa mwezi wa pili bado anakuwa hajafikia hatua ya kuwa mpangaji sugu lakini kuanzia mwezi wa tatu huyu tayari anakwalifai kuwa mpangaji sugu na taratibu za kimkataba zinaweza zikachukuliwa dhidi yake kuondoshwa ndani ya nyumba kama atashindwa kulipa kwa wakati huo”amesisitiza Mndeme
Aidha wito umetolewa kwa Watumishi wa Umma waliohamishwa Vituo vya kazi wakiwa na madeni kulipa madeni hayo ndani ya muda uliotolewa baada ya muda kutisha TBA itafanya Mawaailiano na waajiri wao ili wawasaidie la sivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.


