Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Baraza la Uongozi la Chama cha Sheria Tanganyika (TLS), limelaani vikali vitendo visivyo halali vilivyofanywa na Jeshi la Polisi la Tanzania, ambavyo vimekiuka kwa kiwango kikubwa haki zilizolindwa na Katiba na hadhi ya taasisi za

Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa chama hicho Wakili Boniface Mwambukusi, amesema wamesikitishwa na matukio ya kusikitisha yaliyotokea wakati wa uendeshaji wa kesi ya mwanachama wetu na Kiongozi wa Chama cha siasa cha CHADEMA, Wakili Tundu Antipas Lissu, tarehe 24 Aprili 2025 na 28 Aprili 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Mwambukusi amesema katika kutekeleza wajibu wake wa kikatiba na kisheria wa kulinda utawala wa sheria, kukuza haki, na kulinda heshima ya taaluma ya sheria, TLS inalaani vikali vitendo visivyo halali vilivyofanywa na Jeshi la Polisi la Tanzania, ambavyo vimekiuka kwa kiwango kikubwa haki zilizolindwa na Katiba na hadhi ya taasisi za mahakama.

Amesema uvunjwaji wa sheria na katiba uliobainika ni Uvunjaji wa Haki ya Usawa Mbele ya Sheria na kukamatwa kwa wananchi kwa wingi katika Mahakama ya Kisutu tarehe 24/04/2025 bila kufuata msingi wa kisheria na kwa kuonekana kuzingatia misimamo ya kisiasa ni kinyume na Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.

“Inayolinda usawa mbele ya sheria na kupinga ubaguzi wa kisiasa. ya 14 ya Katiba, inayolinda haki ya kila mtu kuishi na kulindwa na Serikali na jamii. Infinix HOT 121 ambapo wote waliokamatwa katika viunga vya mahakama walinyimwa haki yao ya uhuru kama inavyolindwa na Ibara ya 15’’Amesema.

Amedai kukamatwa huko kulitokea bila sababu za kisheria, bila hati ya kukamatwa, wala kufuata taratibu za sheria,Uvunjaji wa Haki ya Uhuru wa Mtu kwenda Atakako.

“Matendo ya Jeshi la Polisi la Tanzania tarehe 24/04/2025 na 28/04/2025 yalizuia watu kuhudhuria kwa uhuru uendeshaji wa kesi kwenye mahakama ya wazi, kinyume na Ibara ya 17 ya Katiba”Amesema.

Mwambukusi amedai kutotekelezwa kwa Taratibu za Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai,vitendo vya vyombo vya ulinzi na usalama vilikiuka Kifungu cha 186 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Toleo la 2022, kinachothibitisha uwazi wa vikao vya mahakama”Amesema.

Aidha, amedai vifungu vya 11, 12, 14, 21, 23 na 54 vilikiukwa kwa: Kukamata watu bila kuwafahamisha makosa yao,kukosa kuwasilisha hati halali za kukamatwa ni kuwanyima waliokamatwa haki ya kuwasiliana na wakili au jamaa zao.

“Kutumia nguvu kupita kiasi na kusababisha majeraha makubwa. Kufanya upekuzi na ukamataji bila kufuata sheria katika makazi ya mtuhumiwa tarehe 28/04/2025, ambapo familia ya mtuhumiwa iliweza kuzuia uvunjifu huo. Matukio ya tarehe 24/04/2025 na 28/04/2025 yalidhihirisha ukiukwaji wa haki,

Ambapo baadhi ya viongozi wa CHADEMA walizuiwa kwa nguvu kuhudhuria kesi hiyo, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 186 kinacholinda haki ya Wananchi kushiriki katika kesi zinazotakiwa uendeshwa kaatika Mahakama ya wazi”Amesema

Mwambukusi amedai mapendekezo ya TLS kama chombo kikuu cha wataalamu wa sheria ,kilichopewa jukumu la kulinda Katiba, Utawala wa Sheria, na haki za Watanzania wote,

“Wametaka stahiki za kuchukuliwa na namna bora ya kuchukua hatua hizo dhidi ya Askari na wote waliosimamia na kuwezesha zoezi lile batili ,kuandaa kongamano la Kitaifa. Amesema TLS itaandaa kongamano la kitaifa litakalowakutanisha wadau mbalimbali, wakiwemo asasi za kiraia, mahakama, jeshi la polisi, na wawakilishi wa kisiasa kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji wa mamlaka za serikali na kuimarisha mifumo ya kuzuia matumizi mabaya ya madaraka”Amesisitiza.

Mwambukusi amesema kutolewa kwa Miongozo ya Kuzuia Vitendo vya Ukiukwaji wa Sheria, TLS inazitaka Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Wizara ya Mambo ya Ndani kutoa mara moja miongozo na kuimarisha kanuni za ndani zinazokataza ukamataji holela na ukiukwaji wa haki za wananchi mahakamani na katika maeneo ya umma, hasa kwa kuzingatia kuwa mwaka huu taifa linaingia katika Uchaguzi Mkuu.

Amesema uzingatiaji wa Matumizi ya Mifumo ya Mahakama ya Mtandao Kwa mujibu wa kifungu cha 14(1) cha Sheria ya Mahakama za Mahakimu Sura ya 11, Toleo la Marejeo la mwaka 2019, hakimu hataruhusiwa kuchunguza au kusikiliza kosa lolote, kusimamia shauri lolote la madai au kusikiliza rufaa yoyote isipokuwa akiwa ameketi katika Mahakama ya wazi.

“TLS inaonya juu ya matumizi mabaya ya majukwaa ya mahakama mtandaoni. kwa ajili ya kuzuia wananchi kushiriki katika usikilizwaji wa kesi nyeti, hasa za kisiasa kama ya Bw. Tundu A. Lissu”Amesema

Amesema hatua hiyo inaweza kuchochea taharuki na kuharibu imani ya wananchi katika mfumo wa haki, TLS pia inatoa wito kwa Mahakama kuhakikisha kwamba, watu wote wanaofika kwenye viunga vya mahakama wanakuwa huru kushiriki kikamilifu kwenye usikilizwaji wa inashauri mbalimbali na huduma nyingine zote zinazotolewa