Na Heri Shaaban
Kwa Mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, imeeleza kuwa vipindi vifupi vya mvua kubwa inatazamiwa katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Manyara ,Mara,Simiyu , Mwanza ,Mtwara, Lindi na mikoa ya Kusini mwa Pwani ikijumuisha Visiwa vya Mafia.
Aidha Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA imesema Visiwa vya Unguja na Pemba ,Mikoa ya Dodoma na Singida ,Tanga na Dar es Salaam,Kigoma ,Tabora na Katavi,mikoa ya Pwani,ikijumuisha Visiwa vya Mafia, itakuwa na hali ya mawingu mvua ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
Taarifa hiyo imeeleza mikoa ya ,Morogoro,Lindi na Mtwara , Arusha ,Kilimanjaro na Manyara, Rukwa ,Songwe, Mbeya,Iringa,Njombe,na Ruvuma. Kagera,Mara,Geita ,Mwanza, Shinyanga na Simiyu takuwa na hali ya mawingu mvua ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.



