Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka waandishi wa habari
nchini,kufuatilia na kusambaza taarifa sahihi za utabiri na tahadhari ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wa Habari , Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt.
Ladislaus Chang’a ,amesema utoaji wa taarifa sahihi kutoka TMA una lengo la kuhabarisha jamii na kusaidia kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Dkt Chang’a ameshauri waandishi kushirikiana na wataalamu wa sekta
mbalimbali ili kuandaa na kusambaza Makala na Ripoti mbalimbali za hali ya hewa zenye lugha rahisi
Ambazo zitasaidia jamii kutumia taarifa hizo katika kupanga na kukabiliana na athari za hali ya hewa zinazoweza kujitokeza.
Amesema Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo
mengi ya Pwani ya kaskazini pamoja na baadhi ya maeneo ya magharibi mwa ukanda wa Ziwa Viktoria (mikoa ya Kagera na Geita) pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Aidha, mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa katika aeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki na baadhi ya maeneo ya
ukanda wa Ziwa Viktoria (mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu).
Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Februari na ya kwanza ya mwezi Machi , 2026 katika maeneo ya kanda ya Ziwa victoria
“Wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi katika maeneo ya pwani ya kaskazini; na wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Machi, 2026 katika
maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Mei na wiki ya kwanza ya mwezi Juni 2026 katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka”amesema.
Amedai kwa vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao katika baadhi ya maeneo, hususan yanayotarajiwa kupata mvua za Wastani hadi Juu ya wastani.
‘’Mvua za Msimu ambazo utabiri wake ulitolewa mwezi Oktoba, 2025 zilitarajiwa kuwa za Chini ya Wastani hadi Wastani katika maeneo ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida na Dodoma.
Aidha, mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zilitarajiwa katika mikoa Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Mtwara, Lindi, pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.
Mvua hizi zilianza mapema wiki ya nne ya Oktoba na wiki ya kwanza ya Novemba, 2025 katika maeneo mengi ya Magharibi mwa nchi na kufuatiwa na maeneo ya nyanda za juu kusini magharibi wiki ya pili ya mwezi Novemba kama ilivyotabiriwa’’amesema.
Dkt Chang’a amesema msimu wa mvua za Masika mwezi machi mpaka mei 2026
ni mahususi kwa maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), pwani ya kaskazini (kaskazini mwa mkoa wa Morogoro
‘’Mkoa wa Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.
Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi
ya pwani ya kaskazini pamoja na baadhi ya maeneo ya magharibi mwa ukanda wa Ziwa Viktoria (Hususan mikoa ya Kagera, Geita na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma).amesema
Aidha, mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na baadhi ya maeneo ya ukanda wa Ziwa Viktoria (mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na
Simiyu). Ongezeko la mvua linatarajiwa mwezi Aprili, 2026.
Ameongeza kuwa mvua za Masika zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Juu ya
Wastani katika baadhi ya maeneo ya magharibi mwa ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita) pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.
Aidha, mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu.
‘’Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Februari na wiki ya kwanza ya mwezi Machi na kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei 2026.
Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya ukanda wa pwani ya kaskazini.
Mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi na kuisha wiki ya nne ya mwezi Mei na wiki ya kwanza ya mwezi Juni, 2026.
Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi chini ya Wlwastani na zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Machi na kuisha wiki ya nne ya mwezi Mei, 2026.‘‘amesema.
Amesema kwenye miifumo ya hali ya hewa joto la bahari katika eneo la tropiki ya kati ya bahari ya pasifiki linatarajiwa kuwa la wastani
hadi juu kidogo ya wastani
Ambapo hali hii inatarajiwa kuwa na mchango hafifu katika kuimarisha mifumo isababishayo mvua hapa nchini.



