Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma

Bunge la bajeti likiwa linaendelea Dodoma,Waziri wa Fedha,Dkt Mwigulu Nchemba amesema kwa mwaka wa fedha 2025/26, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi ya jumla ya shilingi trilioni 34.10.

Hayo yameelezwa leo Juni 4,2025 jijini hapa wakati akiwalisha makario ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Waziri Mchemba amesema Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 32.31 ni mapato ya kodi na shilingi trilioni 1.79 ni mapato yasiyo ya kodi.

Aidha, Mamlaka itaendelea kuboresha mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa mapato ya serikali ikiwemo TANCIS na IDRAS, pamoja na kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa umma .

Amesisitiza kuwa hayo yote yanafanyika ili kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari na kupunguza upotevu wa mapato unaotokana na udanganyifu wa taarifa za miamala na biashara za magendo.