Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema zaidi ya makampuni 300 yataunganishwa na mfumo wa mfumo wa kisasa wa usimamizi wa kodi za ndani ujulikanao kama “Integrated Domestic Revenue Administration System (IDRAS)” na kutatua kero mbalimbali za huduma za kikodi.
Hayo yalielezwa jana na Kamishna wa Kodi za Ndani, Alfredy Mregi wakati wa mafunzo ya mfumo huo kwa walipakodi wa ndani yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere(JNICC) Dar es Salaam.

Pia Kamishna huyo alisema kwamba kwa kuanzia mnamo Februari 9, 2026 makampuni ama taasisi 60 zitaanza kuingizwa katika mfumo huo ambao unatajwa kurahisisha shughuli za kikodi baina ya TRA na wadau wa kodi za ndani hususani wafanya biashara wadogo wakati na wakubwa.
“Niseme tu kwamba mfumo huu umekuja wakati muafaka kwa ajili ya kutatua kero na changamo za muda mrefu kwa wafanyabiashara wetu wa ndani hivyo utasaidia kupunguza gharama ambazo zilikuwa zikitumika kwa mlipa kodi kuja ofisini na wakati mwingingine kwa TRA kwakuwafuata huko waliko, linguine ni upotevu wa muda na usahihi wake kwakuwa kila kitu kimewekwa kwenye mfumo” alisema Mregi.
Aidha Mregi alisema mfumo huo utaleta tija kwa wadau wa kodi na TRA kwakuwa mfumo huo ni rafiki kwa matumizi na siyo gharama na hivyo kuwaomba wafanyabishara wajifunze vyema na waulelewe kwakuwa una manufaa makubwa ambapo makampuni na taasisi mbalimbali zitaunganishwa na makadirio ya kodi yatakuwa sawiya pasipo uonevu wowote.

Kwa upande wake ,Mwakilishi wa Mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo Pendo Lukasi alisema wanaishukuru TRA kwa mfumo huo utawarahishia kazi kwani kwamaelezo ya mafunzo hayo ni mfumo rafiki.alisema Pendo.
“Mfumo huu ni rafiki kwetu tutawashawishi wafanyabiashara wenzetu kuutumia mfumo huu kwani umekuja kutatua kilio chetu, alisema Pendo.
Mfumo huu umeunganishwa na mifumo ya taasisi nyingineza Serikali ili kurahisisha ubadilishanaji taarifa na hivyo kuboresha utoaji wa huduma kwa walipakodi, na wadauwengine. Mfumo huu unatarajiwa kuanza kutumika rasmi kuanzia mwezi Januari 2026. Mfumo wa IDRASutamwezesha mtumiaji kujihudumia mwenyewe (self-service) akiwa mahali popote na wakati wowote kwakutumia Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).











