Rais wa Marekani Donald Trump amemfukuza kazi mkuu wa idara inayoshughulikia takwimu za ajira baada ya idara hiyo kuchapisha takwimu ambazo kwa mtazamo wa Trump zinavunja moyo
Rais Trump bila ya kutoa Ushahidi wowote amemshutumu Bi. Erika McEntarfer, kwa kuchakachua data za ajira kwa sababu za kisiasa ambazo amesema zinalenga kukichafua chama cha Republican na yeye kama Rais wa Marekani aonekane mbaya, baada ya ripoti mpya kuonyesha nyufa katika soko la ajira la Marekani.
Rais Trump alisema nafasi ya mkuu huyo wa idara inayoshughulikia takwimu za ajira itachukuliwa na mtu mwengine mwenye uwezo mkubwa zaidi.
Ripoti iliyochapishwa na idara hiyo ya takwimu za ajira imebainisha nafasi za ajira zilizoongezeka mwezi uliopita zilikuwa ndogo.
