Rais wa Marekani Donald Trump ameonekana kumuwekea Vladimir Putin makataa ya wiki mbili, akitishia kuchukua mkondo tofauti ikiwa mwenzake wa Urusi bado ataendelea kumrejesha nyuma kwa vitendo vyake.
Wakati Urusi ikizidisha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine, Trump aliulizwa katika Ikulu siku ya Jumatano ikiwa alifikiri Putin anataka kumaliza vita.
“Siwezi kukuambia hilo, lakini nitawajulisha baada ya wiki mbili,” Trump aliwaambia waandishi wa habari huku kukiwa na msururu wa matamshi yaliyotolewa hadharani na Trump akimkosoa Putin.
Tangu Jumapili, Trump amekuwa akiandika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akisema kwamba Putin amekuwa “mwendawazimu” na “anacheza na moto” baada ya Urusi kuzidisha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine.
