RAIS Donald Trump amemshambulia Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa jana Jumatano baada ya kumchezea video iliyoonyesha madai ya mauaji ya kimbari yanayofanywa dhidi ya wazungu.
Rais Trump alisema wakulima hao sasa wanalazimika kukimbilia Marekani ili kunusuru maisha yao.
Trump alisisitiza kwenye mkutano na Ramaphosa kwenye ofisi yake ya Oval kwamba wakulima weupe nchini Afrika Kusini wanalazimishwa kuachia ardhi zao na kuuawa.
Trump alimlaumu Ramaphosa kwa kuwaruhusu wanasiasa weusi nchini humo kuchukua ardhi kinguvu na kuwaua wakulima wazungu, bila ya kuchukuliwa hatua yoyote.
Ramaphosa hata hivyo amekataa madai ya kuwanyang’anya wakulima hao ardhi chini ya sheria mpya ardhi iliyosainiwa mwezi Januari, inayonuia kurekebisha ukosefu wa usawa wa kihistoria wa tangu utawala wa ubaguzi wa rangi.
Mapema mwezi huu serikali ya Trump iliwapa hadhi ya wakimbizi wakilima 50 wazungumzo kutoka Afrika Kusini, licha ya kwamba imesitisha kutoa hifadhi kwa watu wa mataifa mengine.
