Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuchukua hatua kali dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin ikiwa hatokubali kumaliza vita nchini Ukraine.

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuchukua hatua kali dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin ikiwa hatokubali kumaliza vita nchini Ukraine.

Trump amesema Putin anapaswa kujiandaa kwa hilo, ikiwa mazungumzo kati yao katika mkutano uliopangwa kufanyika kesho jimboni Alaska, hayatozaa matunda.Ukraine, Ulaya na Trump waungana kabla ya mkutano na Putin

Kiongozi huyo wa Marekani, kwa mara nyingine amependekeza juu ya uwezekano wa kuwakutanisha rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Putin, mara baada ya mazungumzo ya Alaska.

Hata hivyo, alisema anasubiri kuona jinsi mkutano wake na Putin utakavyomalizika, kwani huenda kusiwe na mkutano mwingine.

Rais Trump anapanga kukutana na Putin jimboni Alaska nchini Marekani, kusaka suluhu ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine ambavyo vimedumu kwa takriban miaka mitatu na nusu.