Rais Donald Trump wa Marekani amesema hakutakuwa na mazungumzo wala makubaliano na utawala wa sasa wa Iran na ameitaka nchi hiyo “isalimu amri” kama sharti kwa Washington kusitisha vita vinavyoendelea.

Trump ametoa ujumbe huo kupitia mtandao wake wa kijamii ambapo pia ameahidi kuisaidia nchi hiyo kuujenga upya uchumi iwapo itakubali matakwa ya Marekani ya kuchagua utawala mpya.

Kiongozi huyomwa Marekani ametoa msimamo huo saa kadhaa baada ya Rais Masoud Pezeshkian wa Iran kusema kwamba “baadhi ya nchi” zimeanza juhudi za usuluhishi wa vita vinavyoendelea bila hata hivyo kutoa maelezo ya kina kuhusu suala hilo.

Serikali ya Iran imekwishasema mara kadhaa tangu kuanza kwa vita kwamba haitokubali kusalimu amri na itaendelea kufanya mashambulizi ya kujibu mapigo hadi pale hujuma za Marekani na Israel yatakapositishwa.