Rais wa Marekani Donald Trump amesema Marekani na Iran lazima zifikie makubaliano na anaamini kuwa makubaliano hayo yanawezekana ndani ya mwezi ujao.

Rais wa Marekani alisema iwapo hakutakuwa na makubaliano, ataingia katika awamu ya pili, jambo ambalo litakuwa chungu sana kwa Iran.

“Lazima tufikie makubaliano, vinginevyo mambo yatakuwa magumu na magumu sana,” aliwaambia waandishi wa habari.

Alipoulizwa iwapo waziri mkuu wa Israel alimtaka kusitisha mazungumzo na Iran, Bw. Trump alisema, “Hatukuzungumza kuhusu hilo.

Nitazungumza nao kwa muda ninaotaka.” Alisema Wairani “walipaswa kukubaliana mara ya kwanza, lakini badala yake walipata Operesheni Nyundo ya Usiku wa manane. … Ikiwa hawatakubali, itakuwa chungu sana kwa Iran.”

Duru mpya ya mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani ilianza Ijumaa iliyopita kwa upatanishi wa Oman mjini Muscat, mji mkuu wa nchi hiyo.