Rais wa Marekani Donald Trump amesema Israel na Iran wamekubaliana kusitisha mapigano, hatua ambayo itaanza kutekelezwa ndani ya saa 24 zijazo na ambayo italimaliza mzozo huu uliodumu kwa siku 12.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema mapema siku ya Jumanne kuwa Israel na Iran zimekubaliana juu ya mpango wa kusitisha kabisa mapigano ambao utaanza kutekelezwa ndani ya saa 24 zijazo.
Kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social, Trump amezipongeza Israel na Iran kwa kuwa na stamina, ujasiri na busara za kuumaliza mzozo huo alioutaja kuwa “Vita vya siku 12”.
Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani amezungumza kwa njia simu na viongozi wa Tehran na kuthibitisha kuwa Iran inaafiki pendekezo hilo la Marekani la kusitisha mapigano, huku Israel ikiwa haijazungumza chochote.
