Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ni ‘hatari’ kwa Uingereza kuwa na ushirikiano wa kibiashara na China.
Hii inajiri wakati ambapo waziri mkuu wa Uingereza yuko katika siku ya tatu ya ziara yake nchini China.
China na Uingereza zilitangaza kuimarisha ushirikiano wao baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer kukutana na rais wa China Xi Jinping.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya mkewe Melania Trump, Trump alisema Rais Xi ni rafiki yake na anamfahamu vyema.
Waziri wa biashara wa Uingereza Bwana Chris Bryant, alisema itakuwa makosa kwa Uingereza kupuuza nafasi ya China katika jukwaa la kimataifa.
‘‘Tumeingia katika mkataba na China tukiwa macho,’’ alisema Waziri huyo akiongeza kuwa Rais Trump anatarajiwa kuzuru China mwezi Aprili.Starmer yuko mjini Shanghai hii leo kabla ya kuelekea nchini Japan kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi.

