Na MwandishinWetu, JamhuriMedia, Tanga

Tume ya Madini inaendelea na kikao kazi cha menejimenti jijini Tanga chenye lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu yake na kuweka mikakati mipya ya kuimarisha Sekta ya Madini nchini.

Kikao hicho kinahusisha Makamishna wa Tume ya Madini, Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi, Katibu Mtendaji wa Tume, Mhandisi Ramadhani Lwamo, Wakurugenzi, Mameneja pamoja na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa.

Kupitia kikao hicho, washiriki wanajadili kwa kina njia bora za kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa, ikiwemo kuimarisha usimamizi, kuongeza thamani ya madini nchini, na kuhamasisha uwekezaji endelevu katika sekta hiyo.

Tume ya Madini imeendelea kuwa chachu ya maendeleo katika Sekta ya Madini kupitia usimamizi madhubuti, utoaji wa leseni, elimu kwa wachimbaji, na ufuatiliaji wa shughuli za madini katika ngazi zote za uzalishaji.