โ€ข Akagua na kuipongeza Serikali kuchukua hatua za haraka

โ€ข Daraja hilo sasa kukamilika

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kigamboni

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe. ๐—›๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ๐—ป ๐—ฆ๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ ameipongeza Serikali kwa hatua za haraka za kurejesha mawasiliano katika Daraja la Nguva ambalo liliathirika na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha changamoto ya uvukaji wa wananchi kwenda upande wa pili.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukagua maendeleo ya ukarabati huo, amsema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na TANROADS wamechukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi wanavuka na kuendelea na shughuli zao kama kawaida. Daraja hilo linaunganisha mawasiliano ya Kata za Somangila na Kimbiji katika eneo la Mwongozo na Gezauole.

โ€œSerikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha mawasiliano yote kwa ujumla yanarejea ambapo hadi kufikia muda huu tayari magari madogo, bajaji, pikipiki na waenda kwa miguu wameweza kuvuka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine hii ni hatua nzuri na tunaipongeza Serikali kwa kutatua changamoto hii kwa haraka,โ€ alisema Mhe. Sanga.

Ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuzingatia taarifa na tahadhari zinazotolewa au kutangazwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza hasa kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.

Kwa upande wake Meneja TANROADS mkoa wa Dar es salaam Injinia Lazeck Kyamba, amesema jitihada za kujaza kifusi ili kufikia usawa wa daraja jipya linalojengwa zinaendelea ili mawasiliano ya njia hiyo yarejee kama awali.

Ujenzi wa Daraja jipya la Nguva unaenda sambamba na Daraja la Kibugumo ambapo gharama zake ni Tsh Bilioni 9.2 fedha zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. ๐—ฆ๐—ฎ๐—บ๐—ถ๐—ฎ ๐—ฆ๐˜‚๐—น๐˜‚๐—ต๐˜‚ ๐—›๐—ฎ๐˜€๐˜€๐—ฎ๐—ป.