Na John Haule, JamhuriMedia, Arusha

Taasisis za kifedha zimeanzishwaa kwa mujibu  wa sheria na zina fanya kazi  za kiuchumi  na kijamii. Taasisi hizi zikiwemo Banki, SACCOS na hata makapuni yanayo toa huduma za mawasiliano ambayo kwa namana nyingine yana fanya kazi za kifedha  mfano M PESA,TIGO PESA.  Hivyo huduma hizi za kifedha ni muhimu sana kwa ustawi wa biashara.

Desturi ya baadhi ya wafanya biashara kuweka fedha kwenye Vibubu au masanduku imekuwa ikizoeeleka sana katika jamii zetu hasa kwenye vikundi vya kusaidiana ili maarufu VIKOBA.


Kiuchumi ili fedha iweze kuwa kwenye mzunguko  in lazma iwekewe bank au kwenye miamala ya kieletroniki kama vile M   PESA .huduma ya lipa namba inayo patikana katika huduma za kifedha inasaidia sana katika kufanya malipo ya kimtandao (electronic payament or transaction).

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba 

Umuhimu wa kuweka fedha kwenye taasisi za kifedha.

Usalama wa  fedha, Kiuhalisia fedha ikihifadhiwa bank  ina  usalama  kwakuwa banki ndio taasisi iliyo pewa idhini kisheria kutunza fedha,hivyo wanannchi hususani wafanya biashara wajenge desturi ya kuweka fedha bank.

Kuongeza mzunguko wa fedha au sarafu. Ili fedha iweze kuzunguka na kutumia lazima iwekwenye banki  maana ikiwekwa kwa vibubu haiwezi zunguka na kupelekea uadimu wa sarafu mitaani.

Fursa za mikopo ya kibiashara na  mikopo kimkakati. Kiuhalisia ili uweze kukopesheka na taasisis hizi za kifedha ni lazma kuwa na Account inayo fanya kazi ,na hata mikopo ya serikali inatolewa kupitia NMB,ya wajasiria mali.

Dhamana za kibiashara mfano kununua hisa  katika makampuni na hati fungani zote hutegemea  taasisisza kifedha hususani bank na saccos ,Soko la hisa dsm stock exchange

Urahisi wa miamala ya kifedha  mfano kupitia Simu za mkonono ,program kama si banking hivyo inarahisisha unnunuzi naa uuzwaji wa bidhaa za kibiashara

Inarahisha  biashara za kimataifa. (international purchasing)  na soko la Africa mashariki   EAC common makert.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutu

SERIKALI INA NUFAIKA PALE WAFANYA BIASHARA WANAPO TUMIA TAASISI ZA KIFEDHA

Inarahisisisha ukusanyaji kodi na mapato ya serikali.ili serikali iweze kueendesha shughuri za Kujenga nchi inaitajika kodi na makusanyo haya yana fanyika toka  vyanzo mbalimbali  hivyo wafanaya biashara wakitumia taasisi hizi za kifedha wana irahishia serikaloi ukpata kodi na mapato yake Kwa mfumo rahisi na wa uhakika. Na hata ufanyaji makadirio ya kodi ya mapato ni rahisi pale miamala inapo fanika kwa kupitia  taasisi za kifedha na hata miamala ya kimtandao yaani electronic transaction

Kuthibiti thamani ya sarafu au inaongeza ustahimilivu wa thamani ya fedha.hii ni kutokana na fedha zote kuwa katika mfumo sahihi  wa ki banki ambao ni rahisi kuthibiti.

Uwezeshaji wanannchi kiuchumi kwa urahisi, kila mwaka tuna ona taasisi hizi zikisaidia jamii mfano kutoa madawati mashuleni, na hata mikopo kwa vikundi  vya wajasiria mali,pia hata serikali inatoa mikopo kwa wajasiria mali kupitia NMB Na hata wana funzi wa vyuo vikuu wana nufaika kupitia taasisi hiz za kifedha,hivyyo ni muhimu wafanfanya biashara ktumia taasisi hizi kibiashara.

UMUHIMU WA TAASISI HIZI KWA JAMII

Zina punguza umaskini katika jamii,hii ni dhahiri kwa taasisis hizi mfano SACOSS  zina wezesha wana chama kutata hata mkopo wa dharura;

Zina punguza changamoto ya ajira mfano uwepo wa mawakala wanao toa huduma za kifedha  za kibanki,na uwakala wa makampuni ya simu wakitoa huduma kifedha.

HITIMISHO
Kwa uhalisia  taasisi za kifedha zote za kiserikali na zile binafsi zina mchango mkubwa kwa uchumi wa Taifa kwa muktadha wa kuhakikisha fedha zina zunguka kwa mujibu wa sheria.

Pia wafanya biashara na wanchi kwa ujumla wajenge desturi ya kutumia taasisi hizi na kujiepusha kuweka fedha kwenye vibubu au masanduku kwa kuwa hio ni tabia inayo weza dhoofisha mzunguko wa fedha ,pia uwekaji fedha kwenye vibubu ni hatari kwa usalama wa kifedha.


Kwa hili ni wajibu wa serikali kuwa elimisha wannanchi kujiepusha kuweka fedha kwenye vibubu  na hata kuweka wazi sheria ya fedha ambayo inatoa zuio kwa mtu kuwa na fedha cash kiasi ambacho hakiruhusiwi.

Wafanya biashara walio wengi hususani hawa  wa kati na wadogo walio wengi  hawana hata acoount banki   kitu amabacho ni changamoto.

Elimu ya fedha na fursa zinazo tolewa na taasisi hizi za jifedha inapaswa kutolewa  kwa wananchi sio tu kupitia vyombo vya habari bali hata mikutano ya umma ikiwemo makongamano ya dini na hata mikutano ya siasa kutengwe hata dakika 15 za kuelimisha umma kuhusu fursa zinazo tolewa na taasisi hizi za kifedha.

IMEANDAKWA NA
JOHN FRANCIS HAULE
MKUU WA SOKO KUU  LA   ARUSHA
0756717987 AU 0711993907