Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia utoaji wa tuzo za kimataifa za Korani katika Uwanja wa Benjamini Mkapa tarehe 5 Aprili mwaka huu.

Rai hiyo ilitolewa na Shekh mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mufti Dkt Abubakari Zuberi, katika ukumbi wa Johari Rotana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, akiwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Tuzo hizo.

Dkt Zuberi amesema wananchi watakaohudhuria na kusikiliza Korani siku hiyo, wajitahidi kuelewa na kuyafanyia kazi yale yote yatakayosomeka katika Korani ili tuweze kupata radhi za Mwenyezi Mungu.

Dkt Zuberi ameishukuru Wizara ya Mambo ya Dini ya Saudia, kwa moyo wake wa kuinua Korani kwa vijana kwa kuamua kufadhili tuzo hizo.

Amesema BAKWATA imeingia mkataba na Saudia, na moja ya malengo hayo ni kuendesha tuzo za Korani na kuinua usomaji kwa vijana.

‘‘Mashindano haya yalikuwa yafanyike katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani, lakini tumeyapeleka mpaka mfumo mosi kwa sababu inasomwa mwezi wowote na mwanadamu anatakiwa kuishi miezi kumi na mbili katika maisha ya Korani.

Mashindano hayo ninayo yazindua leo yanatarajiwa kuanza tarehe 30 Machi na kumalizika Aprili 5 mwaka huu, lengo ni kutoa fursa kwa wananchi wengi kushiriki kuona tuzo hizo na kujionea vipaji mbalimbali
walivyonavyo vijana.

Mwenyekiti wa tuzo hizo, Shekh Othumani Kaporo, amesema mwaka huu baada ya Ramadhani wanatarajia kutoa tuzo za kimataifa ya Korani ili kuwahamasisha vijana wengi kusoma kitabu hicho ambacho ndani yake kinafaida nyingi.

Kaporo amesema, mashindano ya tuzo za kimataifa ya Korani yamepata udhamini mkuu kutoka Wizara ya Dini nchini Saudia.

‘’Mashindano haya hayana tofauti na yaliopita kutakuwa na makundi mawili, kundi la kwanza litakaloshiriki ni la vijana wadogo kuanzia miaka mitano mpaka 12, lingine ni kuanzia hapo mpaka miaka 25’’ amesema.

Amesema mashindano hayo yatahudhuriwa na washiriki 26 kutoka katika mabara yote ya dunia, na mtiririko wa zawadi utatolewa.Tunaaomba wananchi kushiriki kwa wingi kwenye uwanja wa benjamini
mkapa ili kujionea vipaji kutoka kwa vijana wetu’’amesema

Balozi wa Saudia Dkt Yahaya Okash amesema ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Saud Rabia ,ni sehemu muhimu sana katika maswala ya kukuza korani.

‘’Natanguliza shukrani za dhati kwa Rais wa Tanzania ,kwani mashindano haya yanaonyesha ushirikiano mkubwa kati ya wizara ya dini ya Saudia na baraza kuu la waisalamu Tanzania BAKWATA kwa kuweza kushirikiana katika mambo mengi ya kuhakikisha mashindano tuzo hizi yanafanyika .

Nchi ya Saudi Arabia inafanya jitihada kubwa za kueneza korani duniani ,hasa katika mambo yote yanayohusu korani. Mbali na Tanzania Wizara hiyo imekuwa ikisadia ,kusimamia mashindano
mbalimbali makubwa ya korani kwenye nchi tofauti tofauti’’amesema

Wizara imesimamia mashindano ya korani katika nchi 25 tofauti tofauti duniani ,bila shaka mashindano ya tuzo hizi yatakuwa makubwa. Mwenyekiti wa wazee mkoa wa Dar e salaam Shekh Nurdin Matimbwa amesema, jambo la kuandaa tuzo za korani katika mkoa wa Dar es salaam ni kurudisha uhasilia wa mkoa huo kwasababu ulikuwa ni kitovu cha usomaji wa korani .

‘’Sisi kama wazee wa Dar es salaam, tunaona kwa mbali mkoa wetu sasa unataka kurudia katika nafasi yake ya kuwa kinara katika usomaji wa korani. Ni ukweli usiopingika kwamba mji wetu ulikuwa ni kitovu cha usomaji wa Koran,ulikuwa kipindi cha mfungo wa ramadhani ukipita katika mitaa utakuta korani imetawala katika kusomwa na ilikuwa kitovu cha amani na utulivu lakini sasa kumekuwa na mchanganyiko watu ni wengi kiasi cha kusahau asili yake’’amesema.

Amesema kukosa kusimamia maswala yanayohusu dini ,ikiwemo usomaji wa korani kwa vijana ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa maadili.

Amesema miaka ya nyuma hapa Dar e salaam, mtoto kabla ya kupelekwa shule ni lazima aanzie madrasa ndipo apelekwe shule‘’Utaratibu ule ulikuwa na lengo la kuhiadhi koran kwani mungu amekileta tuweze kuhifadhi ,wazazi na walezi wawasihi vijaa nwao waende katika misinghi ya koran si tu kusikiliza bali iwaingie katika viwili wili vyao’’