Ufaransa imetuma ndege za kivita aina ya Rafale juu ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ili kulinda vituo vyake vya kijeshi vya majini na vya anga dhidi ya mashambulizi ya Iran, huku kituo kimoja tayari kikilengwa na droni, Waziri wa Mambo ya Nje Jean-Noel Barrot alisema Jumanne.
“Rafale hizi na marubani wake wamehamasishwa kuhakikisha usalama wa miundombinu yetu,” Barrot aliiambia televisheni ya BFMTV.
“Zimefanya operesheni za kulinda anga juu ya vituo vyetu,” alisema. Kwa mujibu wa waziri huyo, “hanga moja katika kituo cha Ufaransa nchini UAE iligongwa na droni” Jumapili.
Wakati huohuo, Shirika la Habari la Cyprus (CNA) limeripoti kuwa Ufaransa inapanga kupeleka mifumo ya kukinga makombora na droni, pamoja na manowari (frigate), katika kisiwa hicho baada ya kambi ya kijeshi ya Uingereza kushambuliwa kwa droni.
CNA ilisema Rais wa Ufarasa Emmanue Marcon aliwasilisha nia hiyo kwa Rais wa Cyprus Nikos Christodoulides mapema Jumanne.
Cyprus ndiyo nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya iliyo karibu zaidi na Mashariki ya Kati, ambapo mji wake wa Larnaca uko umbali wa takriban maili 129 (kilomita 208) kutoka eneo la karibu zaidi nchini Lebanon.

