KITOWEO cha mchuzi wa Samaki ni mlo mzuri sana kwa wale wasiopenda mboga. Kuna aina nyingi ya samaki wanaopatikana, ikiwa ni pamoja na samaki wa baharini na samaki wa maji safi.

Watu wengi wamekuwa wakila samaki kwa madai kwamba wana mafuta kidogo kuliko kondoo na kuku.Lakini tatizo la samaki ni miiba.

Haijalishi wanataka kula kiasi gani, watu wengi hufikiria mara mbili juu ya kula samaki kwa hofu kwamba watakuwa na miiba.

NAMNA YA KULA SAMAKI MWENYE MIBA

Katika muktadha huu, unapaswa kufanya nini ili kuepuka mwiba wa samaki kunasa kwenye koo lako. Je, unapaswa kula samaki vipi?

Dkt. Kalyani, daktari wa upasuaji na profesa mkuu katika Hospitali ya Serikali huko Vijayawada, alizungumza na BBC kuhusu nini cha kufanya ikiwa mwiba utakwama katika koo lako.

“Wakati wa kula samaki ni vyema kuutoa uti wa mgongo kabla ya kumla, sisi madaktari tunapendekeza vivyo hivyo, iwapo mwiba wa samaki umekwama kwenye koo, ufanyike uchunguzi wa endoscope ili kuutoa, ukishuka kwenye koo hupigwa picha ya X-ray ili kuchunguzwa mahali ulipo na kufanyiwa upasuaji wa kuutoa.

Kesi za aina hiyo hazijaripotiwa katika hospitali ya Serikali ya Vijayawada siku za hivi karibuni,” anasema Dkt Kalyani.

“Ni hatari sana mwiba wa samaki ukikwama kwenye umio, kuna hatari ya kuambukiza kifua kizima, hii inaitwa mediastinitis, ni vyema kuchukua tahadhari kabla ya kula mchuzi wa samaki ili kuepuka hali hii,” anasema.

“Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi mfupa wa samaki unapokwama kwenye koo unaweza kuondolewa kirahisi, pia hakuna haja ya kuwa na wasiwasi ukiingia kwenye umio, hii ni kwa sababu asidi ya tumbo inaweza kuyeyusha mfupa huo wa samaki kwa urahisi.

Jampa Mangamma (54), kutoka Bikkavolu katika Wilaya ya Godavari Mashariki, hivi alikula mchuzi wa samaki kabla ya mfupa wa kitoweo hicho kukwama katika koo lake.

Alikwenda katika Hospitali ya Apollo huko Kakinada akiwa na dhiki kubwa, ambapo madaktari walimfanyia vipimo mbalimbali na kugundua kuwa mfupa wa samaki ulikuwa umekwama karibu na moyo wake.

Hata hivyo, upasuaji huo ulifanyika bila kufungua moyo na bila kuathiri mifupa ya kifua.

Madaktari Sivaramakrishna, Nageswara Rao na Vamsi Chaitanya waliofanya upasuaji huo, waliviambia vyombo vya habari kuwa walitoa mfupa wa samaki uliokwama karibu na moyo wa mgonjwa huyo kwa kutumia utaratibu unaoitwa Traver procedure kupitia mrija.

HATUA ZA KUCHUA MWIBA WA SAMAKI UNAPOKWAMA KOONI

Dkt. Hariharan anatoa mapendekezo.. ‘Ikiwa mfupa wa samaki utakwama kwenye koo, bonyeza kwa nguvu tumbo. Hii itasaidia mfupa kutoka pamoja na hewa.

“Inasaidia kunywa soda mara kwa mara. Gesi iliyo kwenye soda huweka shinikizo kwenye koo, ambayo husababisha mwiba kutoka,” anasema.

Ikiwa tiba hizi za nyumbani hazisaidii, unapaswa kushauriana na daktari mara moja.

Makala haya kwa msaada wa BBC Swahili