Mkuu waTume ya Ulaya, Ursula von der Leyen anasema akiwa Davos kuwa Ulaya imejipanga kukabiliana na Trump kuhusu azimio la Trump kudhibiti Greenland.

Siku ya Jumanne, Rais wa Ufaransa Macron alisema EU inaweza kuzingatia chaguzi kadhaa za kulipiza kisasi ikiwa ni pamoja na “kutunisha misuli ya biashara”.

Wakati huo huo, Rais wa Marekani yuko njiani kukutana na viongozi wa dunia katika mkutano huo lakini anachelewa baada ya Air Force One kulazimika kugeuka kutokana na “suala dogo la umeme”.

Trump anatishia kuongeza ushuru wa asilimia10% kwa “bidhaa zozote na zote” zinazoagizwa kutoka nchi nane za Ulaya kuanzia tarehe 1 Februari ikiwa watapinga pendekezo lake la kutwaa Greenland.