Na Mwandishi Wetu-Jamhuri Media, Moshi
Mbunge mteule wa viti maalum watu wenye ulemavu na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Ummy Nderiananga amesema Rais Samia Suluhu Hassan amewatendea haki watu wenye ulemavu na kuwaomba Watanzania wamchague.
Ametoa kauli hiyo alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika wanja wa Mashujaa mjini Moshi, Oktoba 1, 2025.
Amesema kuwa tangu Rais Samia aingie madarakani mwaka 2021, watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) wamekuwa wakipata huduma za kupaka mafuta bila shida baada ya Serikali fedha za kutosha.
Amesema awamu ya kwanza ilitolewa Sh milioni 60 na zaidi ya watu 5000 wamenufaika.
Amesema ameonyesha utu na kuwafuta machozi watu wenye ulemavu kwa kuwateua na kuwapa wawakilishi katika uongozi wa serikali.
‘Serikali yako inamjali kila mtu na haibagui, umetoa nafasi nyingi za uongozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na viungo.
“Hakkka umetuonesha utu na sisi tunasema utu unalipwa kwa wema, tutakulipa Oktoba 29 bila wasiwasi” amesema.
Amesema Rais amejenga mabweni 188 nchi nzima kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu ili waweze kupata elimu kama watoto wengine.
Amesema katika Wilaya ya Moshi, bweni moja limejengwa kwa gharama kwa gharama ya milioni 80 na kuondoa adha iliyokuwepo.
“Hapa kwetu Moshi kuna bweni moja limejengwa kwa milioni 80 na shule ya bweni kwa wanafunzi wenye ulemavu,sasa nawaomba Watanzania, mtu anayetuonesha anajali, ikifika Oktoba tusimuache,” amesema.
Amesema kabla ya Rais Samia kuingia madarakani, watu wenye ulemavu hawakuwa na ofisi, lakini serikali yake imejenga ofisi zao Dodoma kwa gharama ya Sh milioni 34.
Amesema amekuwa akijali na kuthamani wananchi wa mkoa huo Kwa kutoa fedha yanapotokea majanga.
Amesema ametoa misaada ya zaidi ya Sh milioni 7 nchi nzima.






