Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeyataka makubaliano ya kusitisha vita Gaza yawe ya kudumu.

Baraza hilo vile vile limeikosoa hatua ya Israel ya kutanua udhibiti wake katika Ukingo wa Magharibi kama kitisho kwa juhudi za kupatikana kwa suluhisho la mataifa mawili.

Haya yote yanakuja katika mkesha wa mkutano wa kwanza wa ile “Bodi ya Amani” ya rais wa Marekani Donald Trump ambayo inakutana kujadili mustakabali wa Palestina.

Mkutano huo wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulikuwa umepangiwa kufanyika Alhamis ila ukaahirishwa na kufanywa mapema baada ya Trump kutangaza kuwa mkutano wa hiyo bodi yake utafanyika siku hiyo hiyo, jambo ambalo lingetatiza mipango ya usafiri ya wanadiplomasia ambao pia walistahili kuhudhuria mkutano wa bodi hiyo na huo wa Umoja wa Mataifa