Ikulu ya Urusi Kremlin, imesema hii leo kwamba mazungumzo ya pande tatu yaliyoratibiwa na Marekani huko Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kati ya wajumbe wa Urusi na Ukraine yalifanyika kwa mtazamo wa kujenga.

hIkulu ya Urusi Kremlin, imesema hii leo kwamba mazungumzo ya pande tatuyaliyoratibiwa na Marekani huko Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kati ya wajumbe wa Urusi na Ukraine yalifanyika “kwa mtazamo wa kujenga,” lakini bado “kuna kazi kubwa mbele.”

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari kwamba litakuwa ni kosa kutarajia matokeo makubwa kutoka katika mazungumzo hayo ya awali, lakini ameyasifu kuwa yamefanyika kwa mtizamo wa kujenga hatua ambayo ameitaja kuwa chanya.

Mkutano huo wa siku mbili uliofanyika Abu Dhabi siku ya Ijumaa na Jumamosi ulikuwa mara ya kwanza kwa wajumbe kutoka Moscow na Kyiv kukutana uso kwa uso ili kujadili mpango unaosukumwa na Rais wa Marekani Donald Trump wa kumaliza vita vilivyodumu karibu miaka minne.

Mazungumzo hayo ya pande tatu huko UAE yatafanyika tena Februari Mosi.