Majeshi ya Urusi yameishambulia tena miji miwili mikubwa ya Ukraine mapema leo na kusababisha madhara makubwa kwa majengo na miundombinu ya nishati, lakini hadi sasa hakuna taarifa yoyote ya vifo.

Kwa mujibu wa mkuu wa majeshi wa mji mkuu, Kiev, Tymur Tkachenko, mashambulizi hayo yameharibu jengo moja la kituo cha elimu na jengine la biashara mashariki mwa Mto Dnipro.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Meya Vitali Klitscho, ambaye amesema skuli ya chekechea ndiyo iliyoharibiwa.

Meya wa mji wa pili kwa ukubwa, Kharkiv, Ihor Terekhov, ameripoti mashambulizi kadhaa ya anga yaliyojumuisha makombora na droni, ambapo watu wawili wamejeruhiwa.

Miripuko pia imesikikana kwenye mi wa kusini mashariki wa Sumy, karibu na mpaka wa Urusi.