Jeshi la anga la Ukraine limesema, vikosi vya Urusi viliishambulia nchi hiyo usiku kucha huku milio ya mabomu ikisikika pia katika maeneo mengine ya nchi.
Zaidi ya droni 100 zilionekana zikiruka sehemu tofauti za nchi, huku jeshi la anga likijaribu kudungua baadhi ya droni hizo. Miripuko pia iliripotiwa katika maeneo ya Cherkasy, Chernihiv, Dnipro na Kiev.
Hadi sasa hakuna taarifa za waliojeruhiwa au hasara iliyotokana na mashambulizi yaliyofanywa katika miji hiyo.
Hata hivyo kiongozi wa mji wa Zaporizhzhya Ivan Fedorov, alisema mashambulizi yaliyoshuhudiwa huko yaliwajeruhi watu watatu huku majengo kadhaa yakichomwa moto.
Vyombo vya habari vya Ukraine vimetoa onyo kwa wakaazi kwamba huenda mashambulizi kama hayo ya anga, yakaendelea kushuhudiwa katika siku za hivi karibuni.
