– Vijana Usipime
-Waziri Nanauka apongezwa kuasisi Vijana platform
-Uzalendo watawala kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Kigamboni MC.

Na Byarugaba Innocent, DSM

Mamia ya Vijana kutoka pande zote za Manispaa ya Kigamboni Jijini Dar es Salam wameshiriki kwenye kongamano la Vijana kuelekea Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwenye Manispaa ya Kigamboni Aprili 14,2026 lililokwenda sambamba na uzinduzi wa jukwaa la Vijana Platform uliofanyika leo Aprili 11,2026

Kongamano hili limezinduliwa kwenye Ukumbi wa ‘CH’ wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Col.mstaafu Dkt.Joseph Simbakalia aliyekuwa Mgeni rasmi.

Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa kongamano hilo Dkt.Amon Katunzi aliongoza majadiliano baada ya mada za Umuhinu wa elimu ya uraia katika kujenga mshikamano,Ujenzi wa moyo wa kujitolea na uzalendo kwa Vijana na Taifa lao wakizingatia na kuheshimu utawala wa kisheria zilizowasilishwa na Dkt.Simbakalia na Dkt.Regina Maunde na Bi.Veronica Kiluvia.

Aidha,mada ya Misingi ya maadili,uwajibikaji na uzalendo wa Vijana kwa Taifa lao iliyotolewa na Dkt.Sarah Mwakyambiki na Umuhimu wa kutumia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika maeneo wanakoishi Vijana pamoja na stadi za maisha iliyowasilishwa na Dkt.Euginea Kafanabo zilitosha kuwakumbusha wahudhuriaji wa kongamano Umuhimu wa kutunza amani, maadili, utulivu na mshikamano katika Taifa.

Salama Hassan Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kidete amempongeza Waziri wa Maendeleo ya Vijana Mhe.Joel Arthur Nanauka kwa kubuni uwepo wa Vijana platform kwani linawakunbusha kupambana bila kuchoka kutumia fursa zilizopo ili kuyafikia Maisha wayatakayo.

Godfrey Nyaisa Chacha Mkurugenzi msaidizi akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa sehemu ya Elimu ya Uraia na Uzalendo Suleiman Mvunye amesema Vijana wanapaswa kuwa Wazalendo mara zote kwa Taifa lao kamwe wasitumie mitandao ya Kijamii kuharibu Misingi Bora ya Taifa iliyowekwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Shekhe Abeid Aman Karume waasisi wa Taifa hili.

Kongamano hili lilipambwa na nyimbo za Kizalendo za hayati Kapt.Komba na muziki wa Kizazi kipya kutoka kwa Kala Jeremiah Band -Artist limekuja na Kauli mbiu isemayo “Tanzania ni yetu sote,tushikamane kwa pamoja kuleta Maendeleo

Kwa mujibu wa takwimu za Bi. Veronica Kiluvia mratibu dawati la Vijana Manispaa ya Kigamboni amesema, zaidi ya Vijana 700 kutoka vyuo vikuu,vya kati, Shule za Sekondari sambamba na vijana kutoka makundi mbalimbali wameshiriki.