Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, akiwa pamoja na Viongozi wenzake wa Kitaifa wa Chama hicho, wamewasili Unguja, wakitokea Jijini Dar es Salaam, na kupokelewa na maelfu ya Wanachama, wapenzi, wafuasi na wananchi wa Maeneo mbali mbali Kisiwani humo.
Mapokezi hayo ambayo yamewajumuisha wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Urais wa Zanzibar, yameanzia Bandarini Malindi, na kutamatika katika Viwanja vya Mapinduzi ‘Square’ Kisonge, Mkoa wa Mjini- Magharibi Unguja, ambapo pia walipata fursa ya kusalimiana na kuwashukuru wananchi hao.
Kesho Agosti 10, 2025 viongozi hao watawasili kisiwani Pemba kwa Mapokezi na utambulisho wa wagombea wa nafasi za Urais ambao Agosti 06 mwaka huu, mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho uliwachagua huko jijini Dar es Salaam.











