Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, kimetangaza rasmi majina ya wagombea watakaoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa nafasi za Ubunge wa Majimbo, Viti Maalum na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.
CPA Makalla amesema uteuzi huo, uliofanywa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, umehusisha majimbo 272 upande wa Tanzania Bara na umehitaji umakini mkubwa kutokana na wingi wa maombi ya wagombea.
“Majimbo zaidi ya elfu tano yalipokea maombi ya wagombea,Kazi hii ilikuwa kubwa na ilihitaji umakini mkubwa ,Kwa wale ambao hawajapata uteuzi, tunawaomba waendelee kuwa watiifu kwa chama kwani bado CCM inawathamini,” amesema CPA Makalla.
- Mhe. Mrisho Mashaka Gambo : Arusha Mjini
- Mhe. Emanuel Ole Shangai : Ngorongoro
- Mhe. Mohamed Lujuo Moni : Chemba
- Mhe. Nicodemus Maganga : Mbogwe
- Mhe. Justine Nyamoga : Kilolo
- Mhe. Stephen Byabato : Bukoba Mjini
- Mhe. George Ndaisaba Ruhoro : Ngara
- Mhe. Zuberi Mohammed Kuchauka : Liwale
- Mhe. Pauline Gekul: Babati Mjini
- Mhe. Flatey Maasai : Mbulu Vijijini
- Mhe. Christopher Ole Sendeka : Simanjiro
- Mhe. Vedastus Matayo Manyinyi : Musoma Mjini
- Mhe. Luhaga Joelson Mpina : Kisesa
- Mhe. Godwin Kunambi : Mlimba
- Mhe. Geoffrey Mwambe : Masasi
- Mhe. Cecil Mwambe : Ndanda
- Mhe. Anjelina Mabula : Ilemela
- Mhe. Mansour Shanif Hirani : Kwimba
- Mhe. Hassan Zidadu Kungu : Tunduru Kaskazini
- Mhe. Iddi Mpakate : Tunduru Kusini
- Mhe. Iddi Kassim Iddi : Msalala
- Mhe. George Mwenisongole : Mbozi
- Mhe. Seif Hamisi Gulamali : Manonga
- Mhe. Omar Shekilindi : Lushoto
- Mhe. Januari Makamba : Bumbuli
- Mhe. Alfred Kimea : Korogwe Mjini
- Mhe. Twaha Mpembenwe : Kibiti