Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Arusha

Mpango wa Serikali kuongeza uzalishaji wa Ngano nchini na kupunguza uagizaje nchi za ngano sasa umepata Suluhu baada ya Kampuni ya Balton Tanzania, kuzindua viatilifu 10 vipya kusaidia wakulima wa Ngano, Shiyiri na mazao mengine kukabiliana na wadudu na Athari za mabadiliko ya tabia nchi, ambavyo vinapunguza uzalishaji wa mazao hayo.

Kwa sasa Tanzania inaagiza zaidi ya wastani wa asilimia 90 ya ngano,huku uzalishaji wa ndani ni wastani wa asilimia 10 tu ya mahitaji kwa mwaka.

Akizungumza katika uzinduzi wa viuatilifu hivyo, kwa wauzaji wakubwa wa viuatilifu nchini, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Balton Tanzania, Jacob Vorster alisema viuatilifu hivyo vipya vimetengenezwa kwa teknolojia ya juu kuzuia usugu wa wadudu lakini pia kudhibiti majani ambayo hayahusiani na mazao.

“Balton Tanzania kwa mara ya kwanza tumeamua kuja na viatilifu hivi vyenye ubora hasa kuondoa adha ya wakulima kuendelea kukosa mazao ya kutosha kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi lakini pia uwepo sokoni wa viatilifu ambavyo havina nguvu ya kutosha”alisema

Alisema wakulima ambao watatumia viuatilifu hivyo,wataridhika kutokana na uwezo wake kudhibiti magonjwa, wadudu na majani na vitapatikana maeneo yote nchini kupitia mawakala wao.

Akizungumzia viuatilifu hivyo, Mtaalam wa sayansi ya mimea wa kampuni ya Balton Tanzania ndugu Chonya Wema alisema viuatilifu ambavyo vimezinduliwa ni MWANZO 660SE inapambana na magugu kabla ya kuota mazao na TENO SUPER 75 maalum kwa Ngano na Shayiri. OMEGA 112EC, ambacho kina uakiuadudu aina ya Kimamba,Funzafunza,Inzi weupe ,chorachora,Bokoharamu,Vithiripi, katika nyanya, mahindi, hoho,,vitunguu,matango, kahawa,Ngano na Mpunga.

“pia tumeleta AZOXY plus325EC hii inasaidia kudhibiti Ubwiri Unga,Bakajani,Chelewa na Kutu ya majani na kiuatilifu hiki kinasaidia mazao ya Kahawa,Ngano,Mbogamboga zote,Tikiti maji, maharage na mazao mengine na Tunayo Balton Tebu 250 EC, hii imasaidia sana ukuaji na kudhibiti magonjwa katika Ngano, Shahiri,Kahaw ana viazi Mviringo”alisema

Wema alifafanua kuwa wameleta kiuatilifu ANERIX Extra 76WP, maalum kwa ajili viazi mviringo, mikorosho, mbogamboga na vitunguu,pia wameingiza nchini HALO plus 60 EC hii pia inasaidia pia kudhibiti magonjwa katika Nyanya, Hoho, Vitunguu,Ngano na Mpunga na kuna NICO PLUS 300 OD maaluma kudhibiti wadudu kwenye Mahindi,RIBEME 75 WDG maalum kwa Ngano na Shayiri ,LUZAFEN 250 EC maalum kwa Maharage,

Alisema viuatilifu hivi vinapatikana kwa mawakala kwa bei nafuu na vinatarajia kuongeza uzalishaji wa mazao mbali mbali ya nchini na hivyo kufikia lengo la serikali kuwa na uhakika wa chakula wakati wote lakini pia kusaidia Uchumi wa wakulima nchini.

Baadhi ya mawakala wa Viuatilifu nchini, wakizungumzia viatilifu hivyo, walitaka kusambazwa kwa bei nafuu zaidi na katika ujazo tofauti ili wakulima wengi waweze kununua na kuvitumia na kuachana na viuatilifu visivyo na ubora.

Swalehe Mkilindi wa Moshi mkoa Kilimanjaro,alisema wanaimani viuatilifu hivyo ni mkombozi kwa wakulima nchini ambao wamekuwa wakiapata shida kutokana na ongezeko la wadudu na majani vamizi mashambani.