Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma.
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Profesa Adold Mkenda amesema kuwa kupitia SAMIA SCHOLARSHIP Vijana waliofanya mtihani wa kidato cha sita watakapochaguliwa ambao watapenda kusoma nje ya nchi wanatakiwa kukaa mwaka mmoja ambapo wataweka kambi kampasi ya Nelson Mandera Africa Institute of Teknology kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo uzalendo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelezea mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Waziri wa wizara hiyo Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa pia watajifunza kuielewa nchi yao na namna ya kuitetea huko watakapoenda kusoma.

Amesema kuwa serikali itachukua kuanzia vijana 50 mpaka 100 kwa sharti la kukubali kusoma ndani ya nchi kwa mwaka mmoja ili kufundishwa uzalendo na kuwajengea uwezo kuhusu utamaduni mpya watakaokutana nao nje ya nchi.
Aidha, amesema kuwa kupitia SAMIA SCHOLARSHIP serikali imejipanga kwa ajili ya kuchukua vijana kati ya 650 mpaka 700 watakaofaulu vizuri katika masomo yao na kupata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba.
