Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Shirikisho la Wamachinga Dar es Salaam limeimiza kuwa maamuzi ya wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu kuwa wamejipanga kushiriki kwa kuwa ni haki yao kikatiba.
Katibu wa Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam Agustino Choga ametoa msisitizo huo kuelekea uchaguzi , kuwa wananchi hawawezi kupangiwa na vyama cha kufanya katika uchaguzi huo.
Choga amesema kuwa kila mwananchi mwenyesifa ya kushiriki uchaguzi huo, anayo haki ya kikatiba ya kupiga kura na kufanya maamuzi yake binafsi pasipo kupangiwa na vyama ama mtu yoyote.
Ametoa pongezi kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua shughuli za wafanyabiashara ndogo ndogo na kuwaagiza viongozi wa serikali kuwatambua bila kujali mitaji yao, hali zao .
“Rais Samia alishatupatia Ofisi ya kufanyia kazi na pia kutengewa maeneo rasmi tutakayo tumia hapo baadae ambapo tutakuza zaidi ujasiriamali Wetu na kuzalisha mitaji mikubwa, kwenda madaraja ya juuzaidi ,” amesema Choga.
Katibu huyo pia ametoa pongezi kwa Serikali kwa kutoa fursa ya asilimia 30 kwa makundi ya vijana asilimia 10 , wanawake asilimi 10 wazee asilimia 5 na makundi yenye uhitaji maalumu asilimia 5 kunufaika.
“Tunaishukuru Serikali kwa kutufanyia mambo yote yanayoendelea kujenga amani ya nchi kwa kuwa sisi kupitia umoja wetu tumekuwa na hali ya utulivu kutoka na na serikali kuwa karibu na sisi ,”amesema Choga.
Katibu huyo wa machinga mkoani Dar es Salaam amesema yupo mbio kupitia ama kuangazia changamoto mpya za wamachinga wa mkoa huo huku akitaja sababu yenyelengo kuwa karibu zaidi kuangazia kutoibuka kwa migogoro pasipo uongozi kujua
“Nitapita kila wilaya kuandaa makongamano ambapo hali hiyo itabainisha kama kuna vitu vipya vimeweza kuibuka kwa wakati ilikuweza kufanyia kazi kwa wakati,”amesema Choga.
