Watu 40 wameuawa na wengine 19 kujeruhiwa baada ya wanamgambo wa Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) kushambulia kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk, iliyoko nje kidogo ya mji wa El-Fasher, Darfur Kaskazini mwa Sudan.
Mashirika ya kijamii yanayohifadhi takribani watu 450,000, yamesema wapiganaji wa RSF walivamia makazi na kuwalenga raia wakiwa majumbani mwao. SOMA: RSF yaunda serikali sambamba Sudan
Wanaharakati wa haki za binadamu mjini El-Fasher, unaodhibitiwa na Jeshi la Sudan, wamesema mashambulizi hayo yanaonyesha kiwango cha juu cha ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya raia wasio na ulinzi.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, ameonya kuhusu kuendelea kwa hali mbaya nchini humo, akisisitiza haja ya hatua za dharura za kuzuia madhara zaidi kwa raia.
