OR-TAMISEMI
Wanamichezo kutoka mikoa mbalimbali wanaendelea kuwasili katika viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2025.
Ufunguzi huo unatarajiwa kuongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa leo Tarehe 9 Juni 2025.
Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 yanafanyika kitaifa Mkoani Iringa, ikiwa ni baada ya kufanyika katika Tabora kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2022 hadi 2024.
UMITASHUMTA & UMISSETA inaandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utamaduni na Michezo.
Kauli mbiu ya Mashindano ya mwaka huu ni “Viongozi bora ni msingi wa maendeleo na Taaluma, Sanaa na Michezo, Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu.
