Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Simanjiro

Wanawake wa Mkoa wa Manayara jana Siku ya wanawake Duniani wamemtunukia tuzo Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga, kwa juhudi na umahili wake wa kukuza haki na usawa wa Kijinsia katika Mkoa huo.

Mkuu huyo wa Mkoa alikabidhiwa tuzo hiyo na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mwl.Fakii Lulandala katika maazimisho ya Siku ya wanawake Duniani, iliyofanyika Kimkoa katika Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Mkoani humo.

Wanawake wa mkoa huo pia wamemtunukia tuzo maalum ya utambuzi Katibu Tawala wa Mkoa huo Maryam Ahmed Muhaji kuwa inatambua mchango wake mkubwa katika uratibu na usimamizi wa mipango ya maendeleo na usawa was kijinsia huku akionyeshauongozi thabiti na moyo was dhati katika kusaidia wanawake wa mkoa huo.

Akizungumza na Jamhuri Media Mara baada ya kutunukiwa tuzo hiyo, Sendiga amesema kitendo cha kupatiwa tuzo ni kitendo cha kuthaminiwa kilichofanyika au kinachoendelea kufanyika,hivyo anawashukuru wanawake was mkoa huo kwa kuthamini mchango na kazi anayoendelea kuifanya ndani ya mkoa huo.

” Mimi kama Mkuu wa Mkoa wenu wa Manyara niliyeteuliwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kuja kuwatumikia wananchi was mkoa huu, nasema asanteni kwa kunitunuku hii tuzo, nitaendelea kuwatumikia kwa moyo wangu wote, kwa nguvu,maarifa na juhudi zangu zote nilizopewa na mwenyezi Mungu, hili ni deni ninalotakiwa kuendelea kuwatumikia kwa uadirifu ili kuhakikisha manyara tunasonga mbele kimaendeleo na si vinginevyo, kazi na utu tunasonga mbele,tufanye kazi ndugu zangu” amesema Sendiga.

Aidha mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha wanawake wa Mkoa huo kuhakikisha wanaongeza jitihada katika malezi ya watoto ili kuondokana na utapiamlo, hali kadhalika kuwalea vema waume zao ili nao waweze kua wababa bora katika famia zao, badala ya kuwatenga na muda wote kuonekana ni watu wenye mawazo ya maisha magumu wanayopitia.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa huo Mariam Muhaji akizungumza Mara baada ya kupokea tuzo hiyo amewashukuru akina mama hao kwa kutunukiwa tuzo hiyo muhimu ya kutambua mchango wake kwa akina mama wa mkoa huo.