Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Stephen Wasira amesema mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan ameweka utaratibu mzuri wa Serikali na vyama vya siasa kusikilizana.


Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wakati wa kuhitimisha mkutano wa kampeni za chama hicho kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Oktoba 28,2025.
Amesema kusikilizana huko kumesaidia kuendelea kuwapo na amani na utulivu mkubwa ndani ya nchi.


“Mgombea urais kupitia CCM, Rais Samia ameendelea kuhakikisha Tanzania inakuwa na amani na utulivu kwa kuwa ni njia ya msingi katika kuleta maendeleo na ndiyo shabaha ya chama chetu.


“Rais Samia amekuwa Rais kwa miaka minne na miezi 7, ameingia madarakani kukiwa na majanga kama ugonjwa wa korona uliosababisha kuporomoka kwa uchumi wa nchi na dunia nzima.


“Kkabla ya korona uchumi wetu ulikuwa asilimia 6.9 na ukaanguka hadi asilimia 4 kutokana na janga hili la korona na wakati huo tulikuwa na kilio cha kuondokewa na aliyekuwa Rais Hayati Dk John Magufuli,

“Rais Samia alisema kazi iendele, amefanya kazi kubwa sana ya uongozi na mojawapo ni kwamba alikuja na msamiati na falsafa ya maridhaino ya 4R ili kuleta nchi mahali pamoja, alizungumza na taaisi zote za kidini, kijamii na vyama vya siasa,”amesema.


Amesema Rais Samia aliruhusu mikutano ya siasa pamoja na maandamano kwa vyama vya siasa.


“Rais Samia aliruhusu mikutano ya siasa na maandamano kwa wapinzani ili ajue wanasema nini na wana ajenda gani.


” Ameweka utaratibu wa Serikali na vyama vya siasa kusikilizana ndani ya nchi yetu,
“Kwa uongozi wake aliweza kuinua na kukuza tena uchumi na sasa umefikia asilimia 6 kutoka asilimja 4 ameutoa katika mazingira magumu,”amesema.


Amesema Ilani ya mwaka 2025-30, inaonyesha Tanzania itapiga hatua kubwa ya uchumi wake kukua kutoka asilimia 6 hadi 8.
“Ilani yetu ya 2025-30 ijayo inaonesha tutapiga hatua kutoka asimilia hadi 8 katika ukuaji wa Uchum,”amesema.