Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Vijana, Ajira na Uwekezaji Zanzibar wametakiwa kuwa wawazi ili kuondosha urasimu katika utendaji wa kazi zao.
Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Shaaban Ali Othaman amewataka Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji, kuwa katika utendaji wa kazi zao ili kuondosha urasimu katika sehemu za kazi.

Akizungumza katika ziara ya kukaguwa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo amesema baadhi ya Watendaji wanakuwa sio wawazi katika utendaji wa kazi zao jambo ambalo linasababisha malalamiko kwa Wananchi.
Amesema katika utekelezaji wa majukumu yao ni vyema kuacha urasimu na kuwapatia huduma Wananchi kwa kuzingatia maelekezo yaliowekwa na Serikali.
Hata hivyo amewataka kuwa tTakwimu wakati wa ukusanyaji ili kuondosha mgongano katika sehemu za kazi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Salama Mbarouk Khatib amewataka Viongozi kushirikiana ili kuleta ufanisi wa utendaji wa kazi.

Aidha amewataka kushuka chini kwa Wananchi kusikiliza Changamo zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ili kuondosha malalamiko ya Wananchi.
Ziara hiyo, imeanzia Idara ya Maendeleo ya Vijaana Migombani, Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Zanzibar (ZEEA), Idara ya Ajira na Idara ya Maendeleo ya Vyama vya Ushirika Zanzibar.

