Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam

Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kuwainu qananchi kiuchumi ambapo kwa Mlmwaka wa fedha 2024/2025 ilitenga Tilion 2.44 kwa ajili Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi kiuchumi ambapo zaidi ya watu milioni 18 wamenufaika ambapo wanaume asilimia 51 na wanawake asilimia 49

Akizungumza hayo Oktoba 10, 2025 Kaimu Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Neema Mwakatobe, katika Semina ya kuwajengea uwezo mafunzo hayo yatawasaidia jamii kupata taarifa sahihi kuhusu kazi na majukumu ya baraza hilo, pamoja na kuelewa fursa zilizopo za kiuchumi nchini.

Amebainisha kuwa NEEC ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, na jukumu lake kuu ni kufuatilia na kutathmini shughuli zote zinazofanywa na mifuko mbalimbali za uwezeshaji wananchi kiuchumi zinazotekelezwa na taasisi mbalimbali nchini ikiwemo Mifuko TASAF, Halmashauri,

Hata hivyo amesema Bi. Mwakatobe, Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ilianzishwa mwaka 2004, ikifuatiwa na Sheria ya mwaka 2005 iliyoanzisha rasmi Baraza hilo kwa lengo la kuratibu na kuhakikisha Watanzania wanashiriki ipasavyo katika uchumi

“NEEC hufanya kazi kwa karibu na wizara, taasisi na wadau wa maendeleo wanaotekeleza programu za kuwawezesha wananchi, huku ikihakikisha utekelezaji wa mipango hiyo unawafikia walengwa ili waondokane na Umasikini kwa kupewa mikopo Dhamana “amesema Bi Mwakatobe.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari (JOWUTA), Bw. Selemani Msuya, ameishukuru NEEC kwa kutoa elimu hiyo muhimu kwa wanachama wa chama hicho.

“Tunaishukuru NEEC kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari. Kupitia semina hii, wanachama wetu watakuwa mabalozi wazuri wa kufikisha taarifa za uwezeshaji kwa wananchi,” alisema Bw. Msuya.

Aliongeza kuwa JOWUTA ina wanachama zaidi ya 500 nchini, wakiwemo zaidi ya 150 kutoka mkoa wa Dar es Salaam, na akaomba NEEC kuendelea kutoa mafunzo kama hayo kwa waandishi wa habari wa mikoa mingine ili kuongeza uelewa wa umma.

Aidha ushirikiano huo mpya kati ya NEEC na vyombo vya habari, Wananchi iwananchi wengi zaidi watapata maarifa sahihi kuhusu fursa za kiuchumi, jambo litakalosaidia kukuza ushiriki wao katika kujenga uchumi wao na Taifa kiujumla.