Na Jeremia Mwakyoma- BMH

‎Akiwasilisha mada hiyo katika kikao cha mafunzo kwa watumishi hao Afisa Ulinzi wa TEHAMA na Data wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Ndg. Adelhelm Adrehelm Oddo amesema kuwa mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa watumishi. 

‎”Mitandao, Vifaa vya TEHAMA na mifumo yake  ni vitu vinavyotumiwa na Watumishi kila siku katika utoaji huduma kwa Wananchi na wadau, uendeshaji wa taasisi na kuwasiliana pia, hivyo ni muhimu kuwajengea uwezo ili kusaidia ulinzi na matumizi salama” alibainisha Ndg. Oddo. 

‎Ndg. Oddo aliongeza kuwa katika kikao hiko cha mafunzo wamepata fursa ya kukumbushana juu ya mashambulizi mbalimbali yanayoweza kutokea kwenye mifumo ya TEHAMA, Utunzaji salama wa vifaa vya TEHAMA na mifumo na sheria mbalimbali zinazohusu ulinzi wa mifumo ya TEHAMA na taarifa. 

‎”Ni matarajio yangu kuwa mafunzo yatawaongezea Watumishi kuwa mabalozi katika matumizi salama ya mifumo ya TEHAMA na taarifa” alisisitiza Ndg. Oddo.

‎Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti na Ubunifu wa BMH Bi. Hindu Ibrahim ameshukuru kwa mafunzo waliyopata na kuahidi kuyazingatia ili kuzuia hatari kama za udukuzi. 

‎Nae Daktari Bingwa wa Upasuaji wa BMH Mugisha Nkoronko ameelezea kuwa katika zama za sasa matumizi ya Teknolojia na bidhaa zake yameongezeka sana lakini pia  yana kabiliwa na changamoto kama za udukuzi  na uhalifu mtandaoni hivyo mafunzo hayo yatawawezesha kutambua na kujikinga katika utoaji wa huduma za kila siku za Afya.