Na Salma Lusangi WMJJWW

Wazazi na Walezi wameshauriwa kuacha tabia ya kuwaita watoto majina mabaya au kumtusi matusi yasiyostahili pale ambapo mtoto amekosea kwani tabia hiyo inamuathiri kihisia na kupelekea athari katika mambo mengi ikiwemo ufahamu mdogo katika masomo yake.

Akizungumza katika mafunzo ya Waandishi wa Habari yaliyofanyika mwisho mwa wiki iliyopita Dar es Salaam kuhusu Makuzi, Malezi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Mkufuzi Sharifa Suleiman kutoka Madrasa Early Childhood Zanzibar amesema baadhi ya Wazazi na walezi huwa na tabia ya kuwaita Watoto wao majina ya Wanyama au matusi yasiyostahiki hali ya ambayo inamuathiri mtoto kiakili.

” Niwajibu wa Mzazi na Mlezi kumuonya watoto anapokosea kwa kumuelekeza mema lakini sio kumwita mtoto jina la mbwa, mshenzi, paka, mwanaharamu, wewe sio vizuri kwani inamuathiri kiakili”. Amesema Sharifa.

Amehafamishwa kwamba utafiti wa kisayansi umeonesha kadiri mtoto anavyoathirika kihisia ndivyo ubongo wake unavyoathirika na hatimae husababisha ugonjwa wa Afya ya akili.

Aidha amefamisha kwamba mtoto anahitaji malezi bora tangu mtoto akiwa tumboni kwa kuzingatia mfumo wa mambo yafuatayo; lishe bora, elimu ya mapema, afya bora, Malezi yenye muikito, ulinzi na usalama.

Pia amefahamisha kwamba mifumo hiyo inategemeana katika ukuwaji wa mtoto kwani mtoto anahitaji kukua Kiakili, Kihisia, Kijamii, kimwili na kimaadili.

Naye Mtalaam wa Malezi kutoka Shirika la Children in Cross Fire Denis Gisuka ameeleza kwamba watoto wafundishwe ndani ya siku 1000, kwamaana tangu wakiwa tumboni hadi miaka miwili kwani ubongo wake unashika haraka saana.

Aidha amefahmisha umuhimu wa michezo kwa mtoto inasaidia kujenga ushirikiano, urafiki na mawasilino kati ya Watoto.

Pia michezo hufundisha umuhimu wa kufuata shseria na kuheshumu wengine pamoja na kuongeza uwezo wa kufanya kazi kama timu
” ECD ni malezi ya mtoto tangu siku iliyotunga mimba hadi umri wa miaka 8. Mzazi wahi mapema kabisa kumjenga mtoto katika malezi bora ukishindwa utakula hasara anza mawasiliano na mtoto tangu akiwa tumboni kwani ubongo wa mtoto unashika haraka sana,”. Amesema Denis.

Pia ameeleza umuhimu wa mashirikiano baina ya wazazi wawili baba na mama katika malezi ya mtoto kwani yanajenga upendo kwa pande zote mbili.

Kwa nyakati tofauti akizungumza moja katika ya wazazi Fatma Ali Makame (44) mkaazi wa Rahaleo Unguja, amesema baadhi ya malezi yakurithi ambayo yanamuathiri mtoto lazima wazazi waachane nayo na kufuata mifumo ya kitamu katika malezi.