Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Sekretarieti ya mkataba wa Lusaka (Lusaka Agreement) kuhusu Mkutano wa 14 wa Baraza la Usimamizi wa Mkataba wa Lusaka(LATF) unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Mei 6-8, 2025.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma leo Aprili, 30 2025 Mhe. Chana amesema Tanzania iko tayari kupokea wageni zaidi ya 100 kutoka Nchi wanachama na Nchi waalikwa na kuwahakikishia usalama wao kwa kipindi chote wawapo nchini.

Naye, Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Mkataba wa Lusaka, Bw. Edward Phiri amesema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na tayari viongozi mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Mkataba wa Lusaka wameshathibitisha kushiriki.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii (anayeshughulikia maliasili), CP Benedict Wakulyamba , Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii (anayeshughulikia utalii), Bw. Nkoba Mabula, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Alexander Lobora pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.



