Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amefanya mazungumzo na Balozi wa Burundi, Mhe. Leontine Nzeyimana jijini Dodoma Januari 14, 2026.
Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa karibu kati ya Tanzania na Burundi kwa madhumuni sio tu ya kuimarisha zaidi uhusiano wa kindugu uliopo baina ya nchi hizo, bali pia kusimamia utekelezaji wa miradi ya pamoja ikiwemo ya miundombinu ambayo inalenga kuzifungua nchi hizo kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake.





