📍 Dodoma

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Februari 20, 2026 ameongoza kikao cha kutatua Mgogoro kati ya Wachimbaji Wadogo wa duara No 15 na Uongozi wa Mgodi wa ILILIKA uliopo Nyarugusu Mkoani Geita.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili kupitia wawakilishi wao, Waziri Mavunde amesema ili kufikia muafaka wa mgogoro huo na kuhakikisha haki inapatikana, ameelekeza kupimwa kwa sampuli ya mawe yanayolalamikiwa na pia kutaka uwepo wa mashahidi wengi zaidi wa pande zote ili kupata taarifa sahihi kisha kuendeleza kikao hicho ili haki ipatikane pale inapostahili.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mtendaji Tume ya Madini Mhandisi Ramadhan Lwamo, Afisa Madini Mkazi Geita Mkoa Wa Geita Samweli Shoo, Msimamizi wa Mgodi wa Ililika Bi. Salma Mipawa pamoja na wachimbaji waki wakilishwa na Bw. Geofrey Mushi.