📍Idodi, Iringa

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasili nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Marehemu Mhe. William Lukuvi, Kijiji cha Idodi mkoani Iringa kuongoza waombolezaji kwenye maziko ya Mhe. Lukuvi leo Machi 31, 2026.

Mhe. Lukuvi alifariki dunia tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu.