Waziri Mkuu ashiriki zoezi la upandaji miti Dodoma
JamhuriComments Off on Waziri Mkuu ashiriki zoezi la upandaji miti Dodoma
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 27, 2026 ameshiriki zoezi la upandaji miti, mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa Jijini Dodoma.
Zoezi hilo ni sehemu ya hatua ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo vya kulinda mazingira.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Dkt. Mwigulu akiwa ameambatana na mwenza wake Mama Neema Mwigulu, amempongeza Rais Dkt. Samia kwa uongozi wake kwa kuendelea kudhihirisha namna alivyo kiongozi mwenye maono, mbunifu na anayejali maslahi mapana ya Taifa.
“Shughuli hii imekuwa na utofauti kwa kusababisha miti ipandwe kila kona ya nchi, kwenye vitabu vyetu vitukufu, kupanda mti ni moja ya ibada kwasababu wanufaika wa miti ni wengi” alisema.
Kadhalika, Dkt. Mwigulu ametoa wito kwa Watanzania kuadhimisha siku zao za kuzaliwa kwa kupanda miti. “Tunapokuwa na jambo la kukumbuka la aina hii, tufanye kitu ambacho kinaweka alama na manufaa kwa watu wengine”.
Waziri Mkuu amepanda mtu aina ya MDODOMA/MTIMAJI (Trichilia Emetica).
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akipanda mti mbele ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma Januari 27, 2026 ikiwa ni kuunga mkono, uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake kwa kulinda mazingira. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Kati, PCOI Husna Msagati. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Mke wa Waziri Mkuu, Mama Neema Nchemba akipanda mti mbele ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma Januari 27, 2026 ikiwa ni kuunga mkono, uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake kwa kulinda mazingira. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kupanda mti mbele ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma, Januari 27, 2026 ikiwa ni kuunga mkono, uamuzi wa Rais wa Janmhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake kwa kulinda mazingira. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Kati, PCOI Husna Msagati. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)