Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 31, 2026 ameshiriki kwenye Azania Bank Bunge Bonanza 2026 linalofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya John Merlin jijini Dodoma.

Bonanza hilo limewahusisha Waheshimiwa Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge, Taasisi mbalimbali pamoja na wananchi.

Kaulimbiu ya bonanza hilo ni “UMOJA WETU NI NGUVU YETU.”